Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:44

Afghanistan : Taharuki wakati raia na wageni wakijaribu kuondoka


Wapiganaji wa Taliban wakifanya doria Kabul, Afghanistan, Aug. 19, 2021.

Vurugu na taharuki zimeendelea kushuhudiwa Alhamisi kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Afghanistan wa Kabul wakati maelfu ya raia wa Afghanistan na wageni wakijaribu kukimbia nchi hiyo.

Wakati huo huo viongozi wa mataifa ya Ulaya na Marekani wakitangaza mikakati ya kuwaondoa raia wao pamoja na washirika wao wa Afghanistan wanaotaka kuondoka nchini humo tangu kundi la Taliban kuchukua madaraka mwishoni mwa wiki.

Watu wamekusanyika mbele ya balozi za kigeni mjini Kabul.
Watu wamekusanyika mbele ya balozi za kigeni mjini Kabul.

VOA inaangazia matokeo yanayoendelea leo siku ya uhuru ya taifa hilo lilokumbwa na misukosuko kwa miongo kadhaa sasa.

Mamia ya wanajeshi wa Marekani waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul jana usku kusaidia juhudi za kuwasafirisha maelfu ya Wamarekani, raia wa Ulaya na Wafghanistan wanaoendelea kuwasili kwenye uwanja huo.

Mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Mark Milley amehakikisha kwamba Wamarekani wote wataondolewa kutoka Afghanistan na wanashirikiana na viongozi wa Taliban kuwaondoa.

Jenerali Milley : Wapiganaji wa Taliban wako ndani na nje ya Kabul hivi sasa lakini hawaingilii kati ya operesheni yetu. Kupitia wizara ya mambo ya nchi za nje taliban wanarahisisha kusafiri kwa usalama kwa raia wa Marekani hadi uwanja wa ndege wa Kabul.

Jenerali Mark Milley
Jenerali Mark Milley

Jenerali Milley alisisitiza hayo baada ya kuripotiwa kwamba Wataliban wamekuwa wakiwazuia watu hasa raia wa Afghanistan kuelekea hadi uwanja wa ndege ingawa maelfu wameendelea kukusanyika hapo na wanajeshi wa Marekani walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi hii leo kuwatawanya na kuzuia vurugu.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa shirika la AP mwanamke aliyejitaja ni Fatma anasema maisha yatakuwa magumu chini ya Taliban.

Fatma raia wa Afghanistan anaejaribu kukimbia nchi anaeleza : "Hatuna kaka, hatuna baba, na unafahamu kuishi hapa inakuwa vigumu sana. Tunaishi Herat na tumekimbia huko mimi na dadangu na kufika hapa Kabul pamoja na mama yetu ili kuokoa maisha yetu. Mjomba wetu anafanya kazi na Taliban na anataka kutulazimisha kuolewa, na tayari wamemuambia mama yangu hawezi kuwasomesha wanaume.

Akitetea tena uwamuzi wake wa kuwaondowa wanajeshi wa Marekani bila ya mpango maalum Rais Joe Biden akizungumza na mwandishi wa shirika la habari la ABC, George Stephanopoulos amesema hadhani kulikuwa na hatua nyingine yeyote ya kuchukulwa wakati viongozi wa kisiasa wamekimbia na wanajeshi kuweka silaha zao chini wapiganaji wa Taliban walipoingia.

Rais Joe Biden alisema : "Hapana, sidhani ingeliweza kushughulikiwa kwa njia nyingine, huwenda tukatafakari baadae lakini wazo kwamba kulikua na njia ya kuondopka bila ya kuzusha taharuki si dhani ni jambo lingewezewkana."

Kwa hivi sasa ndege za kwanza zilizosafirisha wakimbizi wa Afghanistan zimewasili Hispania Uingereza na India huku raia wa nchi za Ufaransa Ujerumani, Australia na nyenginezo za Ulaya wameanza kurudi nyumbani.

Wakati huo huo rais wa zamani wa Afghanistan Hamidi Karzai na Mkuu wa Tume ya Upatanishi Abdullah Abdullah wanaripoti kuwa na mazungumzo na viongozi wa Taliban juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais wa zamani aliyekimbilia Umoja wa Falme za Kiarabu Ashraf Ghani amesema anaunga mkono mazungumzo hayo kati ya Taliban na Karzai na wakati huo huo amejitetea tena akisema kwamba alilazimika kukimbia kuepusha umwagikaji damu, na hakuondoka na chechote kama inavyodaiwa, na kwamba anapanga kurudi nyumbani.

Ashraf Ghani rais wa zamani wa Afghanistan : Tuliwasili katika nchi iliyotupokea mikoni mitupu na mtu anaweza kupata taarifa na idara ya uhamiaji ya nchi hii. Msiamini nyinyi raia wa Afghanistan kwamba nimekimbia kuokoa maisha yangu na kukuacheni sikupata hata nafasi ya kuvaa viatu vyangu.

Hali ya maisha inaonekana imeanza kurudi kuwa ya kawaida katika miji mingi lakini wasiwasi umetanda baada ya karibu watu watatu waliuliwa katika mji wa Jalalabad na wapiganaji wa taliban walipokua wanajaribu kuwatawanya waandamanaji wanaopinga utawala wao hapo jana.

Na katika nchi jirani ya Pakistan waziri wa mnambo ya ndani Sheikh Eashid Ahmed amesema hii leo kwamba mamia ya malori yanapita katika vituo viwili vya mpakani, yakiwasafirisha mamia ya wa Afghanistan wanaokimbia nchi yao.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG