Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 16:22

Uganda kupokea wakimbizi kutoka Afghanistan


Hali ilivyokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan Jumatatu Agosti 16, 2021 wakati watu wakijaribu kutoroka nchini baada ya Taliban kuchukua mji huo.
Hali ilivyokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan Jumatatu Agosti 16, 2021 wakati watu wakijaribu kutoroka nchini baada ya Taliban kuchukua mji huo.

Uganda ilisema Jumanne kwamba imekubali ombi la Marenai la kuwapa hifadhi kwa muda, wakimbizi 2,000 kutoka Afghanistan wakikimbia nchi hiyo baada ya udhibiti wa serikali kuchukuliwa na Taliban.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taifa hilo la Afrika mashariki lina hitoria ya miaka mingi ya kupokea watu wanaokimbia mizozo na kwa sasa linawapa hifadhi wakimbizi wapatao milioni 1.4, wengi wao wakiwa kutoka Sudan Kusini.

Esther Anyakun Davinia, naibu wa waziri wa misaada ya dharura, majanga na Wakimbizi amesema Rais Museveni ameridhia ombi hilo lililotolewa Jumatatu na utawala wa Rais Joe Biden.

Davinia alisema Waafghanistan hao watakuwa nchini Uganda kwa muda wa miezi mitatu kabla ya serikali ya Marekani kuwahamishia kwingineko.

Hata hivyo, haikujulikana mara moja ni lini wataanza kuwasili.

Albania na Kosovo pia zimekubali ombi la Mareani la kuwapokea kwa muda, wakimbizi wa Afghanistan.

XS
SM
MD
LG