Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 15:35

Rais wa Afghanistan aahidi kupambana hadi dakika ya mwisho


Rais Ashraf Ghani

Rais Ashraf Ghani amewaambia wananchi wa Afghanistan katika ujumbe wa sauti Jumamosi anakusudia kupigana “vita vilivyowekwa”.

Rais amesisitiza atahakikisha majeshi ya usalama yanatakeleza jukumu wakati ambapo Wataliban wanaonekana kuwa wanakaribia mji mkuu, Kabul, siku kwa siku.

Katika hali ya sasa, kipaumbele chetu cha juu ni kufufua upya nguvu ya vikosi vya usalama na ulinzi vya Afghanistan, alisema katika ujumbe wa dakika mbili na nusu.

Ujumbe huo wa Rais Ghani ulisambazwa kwenye akaunti rasmi za serikali katika mitandao ya kijamii na kurushwa kwenye televisheni ya umma nchini Afghanistan, wakati wa Alasiri.

Ujumbe huo ulifuta uvumi ulioenea huko Kabul kwamba Ghani alikuwa anapanga kutangaza kujiuzulu na kuwaruhusu Taliban kuingia Kabul, kufuatia kundi la wanamgambo kutangaza kusitisha mapigano.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG