Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:18

Blinken afikisha uamuzi wa Rais Biden kwa viongozi wa Kabul


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Mkuu wa Utawala wa Afghanistan Abdullah Abdullah Kabul, Afghanistan Aprili 15, 2021. Picha na High Council for National Reconciliation Press Office/Handout via REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Mkuu wa Utawala wa Afghanistan Abdullah Abdullah Kabul, Afghanistan Aprili 15, 2021. Picha na High Council for National Reconciliation Press Office/Handout via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Antony Blinken ametembelea Afghanistan Alhamisi kwa ziara ambayo haikutangazwa mapema, kwa mazungumzo na viongozi wa Kabul juu ya uamuzi wa Rais Joe Biden wa kuwaondoa wanajeshi wote wa Marekani nchini humo ifikapo Septemba 11, 2021.

Wakati huo baadhi ya wabunge wa Marekani na waatalamu wanatoa maoni tofauti kuhusiana na uwamuzi huo.

Waziri Antony Blinken alikutana kwanza na Rais Ashraf Ghani baada ya kukutana na wanajeshi wa Marekani kwenye ubalozi wa Marekani wenye ulinzi mkali mjini Kabul.

Blinken pia alifanya mazungumzo na mkuu wa Utawala wa Afghanistan Abdullah Abdullah kwa lengo la kuonyesha uungwaji mkono wa Marekani, siku moja baada ya Rais Biden kutangaza kwamba anawaondoa wanajeshi wote wa Marekani nchini humo baada ya miaka 20 ya vita.

Akilihutubia taifa hapo jana Jumatano Rais Biden amesema ana mpango wa kuwaondoa wanajeshi wote 2,500 miezi kadhaa baada ya tarehe ya Mei mosi tarehe iliyowekwa na utawala wa Trump na kukubaliwa na kundi la Taleban.

Biden anaeleza : "Tulikwenda vitani na malengo ya wazi kabisa. Tumekamilisha malengo hayo. Ben Laden ameuliwa na al-Qaida imesindwa nguvu huko Iraq na Afghaniostan. na hivyo wakati umefika wa kumaliza vita visivyo malizika."

Uamuzi wa Biden umesababisha Washirika wa NATO kuharakisha pia kuondoa wanajeshi wake 10,000, pamoja na kuwaitiske serikali ya Ghani inakabiliwa na mapigano makali na wanamgambo wa Taliban.

Baadhi ya Warepublican na waatalamu wanasema uamuzi huo utaweza kukipatia kikundi cha Taliban nafasi ya kuchukua tena udhibiti na kuhujumu maslahi ya Afghanistan na Marekani.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa kigeni kutoka Afghanmistan kumezusha wasi wasi kwamba nchi hiyo huenda sasa ikatumbukia katika vita vikubwa vya wenyewe kwa wenyewe, na kukipatia kikundi cha al-Qaida kujiimiarisha tena.

Waafghanistan wanaeleza wasi wasi kutokana na kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni, mwanafunzi Bilal Sultani anasema : "Hii ni hali ya wasi wasi na watu wanaamini kwamba ikiwa wanajeshi wa kigeni wakiondoka hapa nchini kutakuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. kitu cha kwanza kinahitajika ni amani ya kudumu, maana wa Afghanistan wana hamu ya amani.

Washington imeitisha mkutano wa kutafuta makubaliano kati ya serikali ya Afghanistan na Taliban wiki ijayo huko Uturuki, lakini Taliban imetangaza hii leo kwamba haitohudhuria mkutano huo kutokana na kwamba wanajeshi wa Marekani wanabaki baada ya Mei mosi.

Hapa washington baadhi ya Maseneta wa chama cha Republikan Seneta Mrepublikan Lindsey Graham anasema Rais Biden anafanya makosa kuwaondoa wanajeshi wote huko.

Graham : "Rais Biden kwa bahati mbaya amechagua njia ya hatari kabisa iliyopo ambayo ni kuondokwa kwa njia yeyote ile. Kwa kweli hakuna matokeo mazuri lakini hii ndio njia mbaya zaidi kuliko zote."

Biden amesema Marekani na washirika wake wataendelea mafunzo na kuwapatia vifaa wanajeshi karibu laki tatu wa Afghanistan, kusaidia huduma za dharura na kuendelea na juhudi za kidiplomasia.

XS
SM
MD
LG