Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:24

Marekani, Taliban wafikia makubaliano ya amani ya kihistoria


Mjumbe wa kutafuta amani wa Marekani Zalmay Khalilzad, kushoto, na Mullah Abdul Ghani Baradar, kiongozi wa kisiasa wa ngazi ya juu wa kikundi cha Taliban wakisaini mkataba wa amani kati ya Taliban na maafisa wa Marekani, Doha, Jumamosi Feb 29, 2020.(AP Photo/Hussein Sayed)
Mjumbe wa kutafuta amani wa Marekani Zalmay Khalilzad, kushoto, na Mullah Abdul Ghani Baradar, kiongozi wa kisiasa wa ngazi ya juu wa kikundi cha Taliban wakisaini mkataba wa amani kati ya Taliban na maafisa wa Marekani, Doha, Jumamosi Feb 29, 2020.(AP Photo/Hussein Sayed)

Marekani na kikundi cha Taliban wamesaini makubaliano Jumamosi mjini Doha, Qatar, wakiandaa mazingira kumaliza vita vilivyodumu kwa takriban miaka 19 nchini Afghanistan na hivyo Marekani kurejesha vikosi vyake vilivyoko nchini huko.

Msimamizi mkuu wa mazungumzo hayo Zalmay Khalilzad na Mullah Abdul Ghani Baradar, naibu mkuu wa Taliban katika masuala ya kisiasa, alitia Saini makubaliano hayo wakati wa tafrija fupi katika hoteli moja mjini Qatar ambako Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na mawaziri wa mambo ya nje wengine kutoka nchi kadhaa walihudhuria.

Katika tamko lililotolewa baada ya makubaliano hayo kusainiwa na kikundi cha Taliban, White House ilisisitiza kuwa Rais Donald Trump anatekeleza ahadi yake ya kurejesha vikosi vya Marekani nyumbani kutoka maeneo yenye vita visivyomalizika nje ya nchi na kusimamia kupatikana amani Afghanistan.

“Makubaliano yamefikiwa na Kikundi cha Taliban ambao unaleta makubaliano muhimu ambayo ni ya dharura kuweza kumaliza vita nchini Afghanistan. Wakati kuna kazi inaendelea, hatua hii iliyofikiwa inatoa fursa ya kihistoria kufikia amani,” tamko hilo limesema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mike Pompeo alitoa wito kwa kikundi cha Taliban kuheshimu makubaliano hayo na kuacha mahusiano na vikundi vyenye itikadi kali.

Chini ya makubaliano hayo Marekani itaanza kuwaondoa wanajeshi wake kwa sharti ya kuwa Taliban wazuiye mashambulizi ya kigaidi dhidi ya serikali ya Afghanistan.

Wakati kundi la Taliban likitimiza masharti ya mkataba huo Marekani nayo itaondoa wanajeshi wake wote ndani ya muda wa miezi 14 ijayo.

XS
SM
MD
LG