Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 13:35

Mazungumzo ya amani kati ya Afghanistan na Taliban yaanza


Abdullah Abdullah, katikati, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kitaifa la Usuluhishi la Afghanistan akihudhuria ufunguzi wa mazungumzo kati serikali ya Afghanistan na kikundi chaTaliban, Doha, Qatar, Jumamosi, Septemba. 12, 2020. (AP Photo/ Hussein…

Marekani imezishinikiza pande hasimu nchini Afghanistan Jumamosi kuelekea katika mazungumzo yao ya kwanza ya amani ana kwa ana kwa nia ya kufikia makubaliano ya kushirikiana madaraka ambayo yatashirikisha “fikra zinazoshindana” na kumaliza kabisa miongo kadhaa ya umwagaji damu nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ametoa matamshi hayo katika tafrija maalum huko Doha, Qatar, kuashiria kuanza kwa majadiliano ya kutafuta suluhu yanayosimamiwa na Marekani, yajulikanayo kama mashauriano ya ndani ya Afghanistan kati ya ujumbe wa waasi wa Taliban na serikali ya Afghanistan.

Mike Pompeo
Mike Pompeo

“Leo hii hili ni tukio lenye msukumo wa kweli. Wananchi wa Afghanistan hatimaye wamechagua kukaa pamoja na kuunda muelekeo mpya kwa nchi yenu. Hii ni fursa ya kuwa na matumaini,” Pompeo amesema.

Ametahadharisha kuwa mazungumzo haya ya yaliyopewa jina la Intra-Afghan ‘bila shaka yatakabiliwa na changamoto nyingi’ kwa sababu ya miongo kadhaa ya migawanyiko, lakini pande zote mbili zinatakiwa kuwa “wavumilivu” ili kuchukua fursa hii ya kuandika upya historia ya Afghanistan.

“Nimatumaini yetu kuwa sehemu hii ni moja maridhiano na maendeleo, na siyo simulizi nyingine ya vilio na umwagaji damu. Tunawataka mfanye maamuzi yatakayowaepusha na vita na ufisadi kuelekea kwenye amani na maisha bora,” amesisitiza Pompeo.

Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani amesema kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo Marekani imesaini na Taliban Februari 29, yaliwezesha kuanza kwa mashauriano ya Jumamosi kati ya pande hasimu zinazopigana nchini Afghanistan.

Wakati akisema ilikuwa kwa wananchi pekee wa Afghanistan kuamua mustakbali wa mfumo wa kisiasa utakaoongoza nchi yao, Pompeo aliongeza kusema alikuwa na matumaini matokeo ya mazungumzo hayo yataheshimu haki za wananchi wote wa Afghanistan na kulinda maendeleo ya kijamii yaliyofikiwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

"Wakati mnafanya maamuzi yenu, lazima mzingatie kuwa chaguo na mwenendo wenu utaathiri vyote ukubwa na upeo wa msaada wa Marekani utakaotolewa siku za usoni. Matumaini yetu ni kuwa mtafikia amani ya kudumu, na lengo letu ni ushirikiano wa kudumu,” amesema Pompeo.

Abdullah Abdullah, kiongozi wa ujumbe wa Afghanistan, amesema katika uzinduzi wa tafrija hiyo kuwa timu yake imekuja Doha “ na nia nzuri na makusudio mema” kufanya mazungumzo na Taliban kumaliza umwagaji damu uliodumu kwa miaka 40.

Mazungumzo ya amani ya Afghanistan yakiendelea Doha, Qatar.
Mazungumzo ya amani ya Afghanistan yakiendelea Doha, Qatar.

“Tumekuja kufanikisha amani ya kudumu na yenye heshima. Hakuna mshindi kupitia vita na matumizi ya kijeshi, lakini hakutakuwa na upande utakaoshindwa iwapo mgogoro huu utatatuliwa kwa maridhiano ya wananchi wetu,” amesema Abdullah mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kitaifa la Usuluhishi la Afghanistan.

Mullah Abdul Ghani Baradar mkuu wa ujumbe wa Taliban, ameahidi katika hotuba yake kwamba timu ya mazungumzo ya waasi itaingia katika mazungumzo ya Intra-Afghan “kwa dhati kabisa” na kusisitiza kwa pande zote mbili kuendelea mbele kwa kuvumiliana.

“Tunauhakikishia ulimwengu tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wertu kufanikisha mazungumzo yenye tija ya Intra-Afghan.

Tunataka Afghanistan ambayo ni yenye kujitegemea, yenye maamuzi yake, iliyoungana, yenye maendeleo na huru – Afghanistan yenye mfumo wa Kiislam ambao watu wote wa taifa hili watashiriki bila kubaguliwa,” Baradar amesema.

Pompeo baadae alifanya mikutano na kila upande peke yao alipokutana na Baradar na Abdullah, ambapo wajumbe wa mazungumzo haya walishiriki.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG