Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:53

Maafisa wa usalama walitaarifu bunge juu ya shutuma dhidi ya Russia


Paul Nakasone
Paul Nakasone

Maafisa wa juu wa idara ya ujasusi ya Marekani Alhamisi wanatarijwa kufika katika kikao cha faragha mbele ya viongozi wa wabunge kueleza kile wanachojua kuhusu shutuma za njama za Russia kuwalipa wanamgambo wa kundi la Taliban, ili wawashambulie wanajeshi wa Marekani na washirika wao huko Afghanistan.

Ikulu ya Marekani White House imethibitisha kwamba Mkurungenzi wa Idara ya Ujasusi,CIA, Gina Haspel na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Paul Nakasone, watakutana na kundi la wabunge wanaojulikana kama Gang of Eight.

Mkutano huo utawapa fursa ya kwanza wabunge kusikiliza maelezo moja kwa moja kutoka kwa maafisa wa ujasusi waliobobea juu ya madai hayo.

Shirika la habari la Reuters likinukuu vyanzo vya serikali ya Marekani na nchi za Ulaya, vinaripoti kwamba Marekani hivi karibuni ilipata ripoti ya ujasusi ambayo inathibitisha madai hayo ya Russia kutoa pesa na vifaa vya kijeshi kwa Taliban ili kushambulia wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa jeshi la ushirika.

Lakini Trump amekanusha madai hayo, na jana aliandika kwenye ukurusa wake wa Twitter kwamba habari hiyo ya mpango wa Russia kuwaua wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan ni uzushi.

Kwa upande wao maafisa wa kundi la Taliban nao wamejitokeza na kuthibitisha mpango huo.

Kamanda wa Taliban Ghazni Moulani Baghdadi ameliambia gazeti la Business Insider kwamba, makamanda wa Taliban wamekuwa wakipokea pesa na vifaa vya kijeshi kutoka kwa idara ya ujasusi ya Russia.

XS
SM
MD
LG