Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:12

Milipuko mitatu yauwa watu zaidi ya 52 Ethiopia


Haacaaluu Hundeessaa
Haacaaluu Hundeessaa

Zaidi ya watu 52 wameuawa katika jimbo la Oromiya nchini Ethiopia katika maandamano ya kupaza sauti dhidi ya mauaji ya mwanamuziki Haacaaluu Hudneessaa aliyepigwa risasi Jumatatu usiku katika kile polisi wanasema ni shambulio la makusudi.

Msemaji wa jimbo hilo Getachew Balcha ameeleza kuwa watu waliokufa ni waandamanaji na maafisa wa usalama. Hali kadhalika taarifa hizo zinaeleza kuwa baadhi ya maduka ya biashara yamechomwa moto.

Maandamano na ghasia zilizuka kuanzia Jumanne katika miji kadhaa ya jimbo la Oromiya na katioka mji mkuu wa Addis Ababa inaripotiwa kwamba afisa mmoja wa polisi ameuawa na idadi ya watu wasiojulikana kufariki baada ya kutokea milipuko mitatu wakati wa maandamano.

Vyanzo vya habari nchini Ethiopia vimeeleza kuwa mwanasiasa wa upinzani Jawar Mohamed anashikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo pamoja na watu wengine 34.

Nayo Serikali ya Ethiopia imethibitisha kwamba kiongozi huyo maarufu wa upinzani nchini humo Mohammed amekamatwa. Mohammed ambaye hapo awali alikuwa mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari na aliyejiunga hivi karibuni na chama cha Oromo Federalist Congress.

Wakati huo Mkuu wa polisi nchini Ethiopia Endeshaw Tassew amesema kwamba Mohammed alikamatwa baada ya kutokea hali ya kutoelewana na polisi juu ya kifo cha mwanamuziki huyo.

XS
SM
MD
LG