Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:09

Marais walioko madarakani jumuiya ya EAC hawakuhudhuria maziko ya Nkurunziza


Maziko ya kitaifa ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Maziko ya kitaifa ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Hakuna rais wa Afrika Mashariki ambaye yuko madarakani aliyehudhuria mazishi ya Marehemu Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Nkurunziza yaliyofanyika Ijumaa, gazeti la The East African limeripoti.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa wakati akiwa madarakani, Nkurunziza alitengwa kidiplomasia baada ya 2015, wakati alipoamua kugombea urais kwa muhula wa tatu ulioibua maandamano kupinga hatua hiyo.

Rais wa Tanzania John Magufuli alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliyekuwa amefuatana na ujumbe wa watu 21, akiwemo rais mstaafu Jakaya Kikwete na mkewe, Salma Kikwete.

Naye Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Ken Obura.

Uganda iliwakilishwa na Matayo Kyaligonza, balozi wa nchi hiyo nchini Burundi.

Hata hivyo, haikujulikana iwapo jirani wa Burundi, Rwanda ilikuwa imetuma mwakilishi yeyote rasmi.

Lakini wiki iliyopita, Rais wa Rwanda Paul Kagame alituma salamu za rambirambi na kuamuru bendera kurushwa nusu mlingoti, akiashiria kuwa atatumia fursa hiyo kuondoa tofauti na jirani yake Burundi.

Sudan Kusini haikupeleka mwakilishi, lakini Rais Salva Kiir katika salamu zake za rambirambi alimuelezea Nkurunziza kama kiongozi aliyesimama bega kwa began na wapiganaji wa SPLM/A wakati wa harakati za ukombozi uliopelekea uhuru wa Sudan Kusini.

“Nkurunziza alikuwa kiongozi bora wa Afrika Mashariki ambaye kifo chake ni pengo kubwa kwa eneo hilo,” amesema Rais Kiir.

Nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki ziliamrisha bendera zao kupeperushwa nusu mlingoti kufuatia kifo cha Nkurunziza Juni 8.

Na kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22, Burundi ilipiga kura kuchagua waziri mkuu, nafasi ambayo ilitenguliwa huko nyuma na katiba ya zamani ya nchi hiyo.


XS
SM
MD
LG