Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:36

Wapiganaji wa Taliban waendelea kufanya doria katika mitaa ya Kabul


Wapiganaji wa Taliban wakilinda mbele ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai mjini Kabul, Afghanistan, Jumatatu, Agosti 16, 2021.(AP Photo/Rahmat Gul)
Wapiganaji wa Taliban wakilinda mbele ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai mjini Kabul, Afghanistan, Jumatatu, Agosti 16, 2021.(AP Photo/Rahmat Gul)

Wapiganaji wa Taliban waliendelea kushika doria katika mitaa ya Kabul Jumatatu, siku moja baada ya kundi hilo kuingia katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na Rais Ashraf Ghani kuondoka nchini.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana kujadili maendeleo hayo, wakati Marekani na zaidi ya nchi nyingine 60 zilitoa taarifa zikitaka pande zote nchini Afghanistan kuwaruhusu raia wa Afghanistan au wa kigeni kuondoka nchini humo ikiwa wanataka.

Marekani ilituma wanajeshi zaidi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul wa Hamid Karzai kusaidia kuwaondoa wanadiplomasia wa Marekani na washirika wa Afghanistan. Mataifa mengine ya Magharibi pia yalifanya kazi Jumatatu kuwatoa wafanyakazi wao nje ya nchi hiyo.

Maelfu ya raia wa Afghanistan pia wamejazana kwenye uwanja wa ndege, wakihofia kurudi kwa utawala wa Taliban lakini wanakabiliwa na njia isiyo wazi ya kutoka.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Afghanistan ilitoa taarifa leo Jumatatu asubuhi ikisema upande wa raia wa uwanja wa ndege umefungwa hadi hapo itakapotangazwa tena.

XS
SM
MD
LG