Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:13

Habari za kutatanisha zashamiri juu ya Taliban kuingia au kushambulia Kabul

Moshi ukionekana karibu na Ubalozi wa Marekani mjini Kabul, Afghanistan, Jumapili, Agosti 15, 2021. Wapiganaji waTaliban fighters wakiingia katika nje ya mji mkuu wa Afghanistan, huku wafanyakazi wa serikali wakikimbia ofisi zao.

Maafisa katika mji mkuu wa Afghanistan wa Kabul ambao umekumbwa na wasiwasi, pamoja na Taliban wote wanakanusha ripoti kwamba waasi wameingia au wameushambulia mji huo.

Hata hivyo ripoti nyingine zinasema Taliban wameanza kuingia Kabul kutoka pande zote wakinukuu maafisa wa serikali na mashuhuda.

Ayesha Tanzeem mwandishi wa VOA mjini Kabul, amesema kulikuwa na taharuki katika mitaa ya jiji, wakati Habari ziliposambazwa kwamba Taliban waliingia mji mkuu.

Mwandishi wa VOA nchini Afghanistan, alikuwa katika ofisi ya uhamiaji wakati kila mtu alipoambiwa aondoke mara moja aende nyumbani.

Barabara katika mitaa ya Kabul, zilikuwa na msongamano wakati watu walipopata taharuki kurudi nyumbani au kwenda kwa familia zao.

Hata hivyo anaripoti kwamba mambo yanarudi pole-pole katika hali ya kawaida, lakini kuna msongamano mkubwa barabarani.

XS
SM
MD
LG