Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:04

Mwanadiplomasia wa Marekani aeleza machungu ya kuanguka kwa mji wa Kabul


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani ameeleza hatua ya Taliban kuichukua Afghanistan na kuanguka kwa mji wa Kabul “ni mambo yenye kuumiza moyo,” na anasema majeshi ya Marekani yanashughulikia kuwaondoa kutoka nchini humo Wamarekani wote, na pia Waafghanistan waliokuwa wakifanya kazi na Marekani, 

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema Jumapili usalama wa wafanyakazi wa Marekani, ambao baadhi yao bado wako ubalozini, na wasaidizi wao raia wa Afghanistan ni “jukumu lao la kwanza,” akipinga ukosoaji kwamba Washington ilikuwa haijajitayarisha kwa tukio la kuanguka kwa majeshi ya Afghanistan kwa haraka.

Marekani itafanya “kila tunaloweza kwa kadiri itakavyo kuwa kuwaondoa wote hao nje ya Afghanistan iwapo hilo ndilo wanataka,” Blinken ameiambia kipindi cha CNN cha State of the Union.

“Hatujawaomba Wataliban kitu chochote,” Blinken ameongeza. “Tumewaambia Wataliban kuwa iwapo wataingilia shughuli za wafanyakazi wetu, na operesheni zetu, wakati tukiendelea kujiondoa nchini humo, kutakuwa na uamuzi wa haraka dhidi yao.”

Siku ya Jumapili kando ya shughuli hizo, afisa wa Marekani, akizungumza kwa sharti asitajwe jina lake kutokana na unyeti wa hali halisi iliyoko, ameiambia VOA shughuli za kuwaondoa wafanyakazi wa ubalozini Kabul “zinaendelea vizuri.”

Afisa huyo pia amesema kuwa maelfu zaidi ya wanajeshi wa Marekani wanawasili nchini Afghanistan na “wamedhibiti kikamilifu” maeneo yanayo zunguka ubalozi na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, nje ya mji wa Kabul.

Afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani ameiambia VOA kuwa Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye amekuwa katika mapumziko kwa siku kadhaa zilizopita huko Camp

David, sehemu ya mapumziko ya rais nje ya Washington, amekuwa akipewa taarifa juu ya yale yanayoendelea kutokea hivi sasa.

“Rais amezungumza na wajumbe wa timu ya Usalama wa Taifa juu ya hali ya Afghanistan na ataendelea kupewa taarifa za hivi sasa na kuendelea kupewa habari siku nzima,” afisa huyo amesema, akitaka jina lake lisitajwe.

Biden siku ya Jumamosi aliidhinisha wanajeshi zaidi 1,000 kupelekwa Kabul kusaidia kuuhami ubalozi na mali na kuwawezesha wafanyakazi wa Marekani na Waafghanistan waliokuwa wanafanya kazi kwa ajili ya Marekani kuondoka salama.

Jumla ya wanajeshi 4,000 wanatarajiwa kuwasili Kabul katika siku sijazo, kuongeza nguvu kwa idadi ya wanajeshi wa Marekani iliyokuwa imefikia 650 katika

XS
SM
MD
LG