Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:32

Zoezi la kuwatafuta manusura wa tetemeko la ardhi Indonesia laendelea


Wafanyakazi wa uokoaji wkaitumia msomeno kufikia mwili wa muhanga wa tetemeko la ardhi aliyekuwa chini ya kifusi katika mji wa Cianjur, magharibi ya Java, Indonesia, Nov. 22, 2022.
Wafanyakazi wa uokoaji wkaitumia msomeno kufikia mwili wa muhanga wa tetemeko la ardhi aliyekuwa chini ya kifusi katika mji wa Cianjur, magharibi ya Java, Indonesia, Nov. 22, 2022.

Wafanyakazi wa uokoaji  nchini  Indonesia waliendelea  Jumanne kuwatafuta manusura wa  tetemeko kubwa la ardhi kupiga kisiwa kikuu cha Java.

Shirika la kikanda la kusaidia maafa katika mji wa Cianjur limeripoti kuwa vifo kutokana na tetemeko hilo vimeongezeka na kufikia 252, huku mamia wakiwa wamejuruhiwa na watu 31 hawajulikani waliko.

Gavana wa Java Magharibi, Ridwan Kamil alisema baada ya tetemeko la Jumatatu kuwa zaidi ya watu 13,000 ambao nyumba zao zilikuwa zimeharibiwa vibaya sana walisafirishwa kupelekwa katika vituo vya uokoaji.

Mamia ya watu waliojeruhiwa walikimbilia mitaani katika mji wa Cianjur kufuatia tetemeko hilo, wengine wakiwa wametapakaa damu na kifusi. Kituo cha Utafiti wa Jiolojia cha Marekani kilisema Cianjur ndio kitovu cha tetemeko lenye ukubwa wa 5.6 kwa kipimo cha rikta.

Mtikisiko ulihisiwa katika mji mkuu, Jakarta, ambao uko umbali wa kilomita 70, ambapo watu waliokuwa katika majengo marefu pia waliondolewa.

“Wengi wa wale waliofariki walikuwa watoto,” Kamil alisema. Alisema wengi walikuwa wanafunzi wa shule za umma waliokuwa wamemaliza masomo ya kawaida kwa siku ile na walikuwa wanachukua mafunzo ya ziada katika shule za Kiislam. Cianjur inajulikana kwa kuwa na shule nyingi za mabweni na misikiti.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG