Biden anahudhuria mkutano wa G-20, ambapo rais wa taifa hilo Joko Widodo ni mwenyeji wa mkutano huo. Katika mazungumo yake na Widodo pembeni ya mkutano huo, Biden amemtania na kusema kwamba “ sidhani nataka kurejea kwetu tena.
” Kikao cha viongozi hao kinaonkeana kupunguza taharuki ya kidiplomasia kati ya Washington na Jarkata, kabla ya mkutano wa G-20 unaozileta pamoja nchi wanachama 20 wenye nguvu ulimwenguni.
Hilo linafanyika wakati macho yakiwa yameelekezwa kwenye vita vya Ukraine, kukiwa na shinikizo la kuitenga Russia kutoka mataifa ya magharibi.
Rais wa Russia Vladimir Putin hatahudhuria mkutano huo, na wala haijabainika iwapo atashiriki kwa njia ya mtandao. Hata hivyo mwenzake wa Ukraine Volodmyrr Zelenskyy atahurudhuria kwa njia ya mtandao. licha ya kuwa Ukraine siyo mwanachama wa G-20.