Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:12

Indonesia: Watoto 32 wafariki katika mkanyagano katika uwanja wa kandanda


Ramani ya Indonesia
Ramani ya Indonesia

Watoto 32 walifariki katika ajali mbaya iliyotokea katika uwanja wa michezo nchini Indonesia, afisa mmoja amesema Jumatatu huku polisi wakichukua hatua ya kuwaadhibu wahusika katika moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya kandanda.

Janga hilo la Jumamosi usiku katika mji wa Malang lilisababisha vifo vya watu 125 na wengine 323 kujeruhiwa baada ya maafisa wa usalama kufyatua mabomu ya kutoa machozi katika uwanja uliokuwa umejaa ili kuzima uvamizi wa uwanjani, na kusababisha mkanyagano.

Darzeni ya watoto waliojikuta katikati ya mkanyagano huo walipoteza maisha, afisa katika wizara ya kulinda watoto na kuwawezesha wanawake ameiambia AFP.

Huku hasira dhidi ya polisi zikiongezeka, waziri wa usalama wa Indonesia Mahfud MD ametangaza kwamba kumeundwa kikosi kazi kuchunguza tukio hilo na kuomba waliohusika kuadhibiwa.

“Tunaomba polisi kubaini ni nani waliotekeleza uhalifu huo na kuwachukulia hatua pia tunatumai watatathimini taratibu zao za usalama,” amesema katika taarifa kwenye vyombo vya habari.

Jeshi la polisi limemfukuza kazi mkuu wa polisi katika mji wa Malang saa chache baada ya hotuba ya waziri wa usalama.

Idara ya polisi mashariki mwa mji wa Java imewasimamisha kazi maafisa tisa kwa maagizo ya polisi ya taifa, msemaji wa polisi Dedi Prasetyo ameuambia mkutano wa waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu jukumu lao katika janga hilo.

XS
SM
MD
LG