Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:26

Mamia waadhimisha miaka 20 ya tukio la kigaidi la Bali


Waltu waliokusanyika kwa ajili ya sala ya kumbukumbu ya waliofariki katika shambulizi la kigaidi la mwaka 2002 na kuuwa watu zaidi ya 200 Oktoba, 12, 2022.
Waltu waliokusanyika kwa ajili ya sala ya kumbukumbu ya waliofariki katika shambulizi la kigaidi la mwaka 2002 na kuuwa watu zaidi ya 200 Oktoba, 12, 2022.

Mamia ya watu walikusanyika Jumatano katika kisiwa cha kifahari cha Indonesia cha Bali, kukumbuka miaka 20 toka kutokea kwa milipuko miwili ya mabomu.

Mashambulizi hayo yaliuwa watu 202 wengi wao wakiwa ni watalii wa kigeni ikijumuisha raia 88 wa Australia na Wamarekani saba.

Ibada zilifanyika mfululizo katika maeneo kadhaa nchini Australia na uwakilishi wa Australia wa Bali katika mji wa Denpasar, ambapo walio nusurika katika shambulizi la kigaidi la mwaka 2002.

Ndugu, jamaa na marafiki wa waliofariki dunia walikuwa miongoni mwa watu 200 waliohudhuria katika ibada ya kumbukumbu.

Walio nusurika bado wanaendelea kusumbuliwa na hali ya wasiwasi kutokana na shambulizi la Jumamosi usiku katika mwezi wa Oktoba mwaka 2002.

Tukio hilo lilitokea baada ya gari lililokuwa na mabomu katika klabu ya Sari na mabomu ya kujitoa muhanga karibu na kilabu cha pombe cha Paddy kulipuka.

XS
SM
MD
LG