Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:40

Milango ya uwanja ilikuwa imefungwa katika maafa ya Indonesia

Rais wa Indonesian, Joko Widodo na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu cha Indonesia Mochamad Iriawan walipotembelea uwanja wa mpira wa miguu wa Kanjuruhan wa Malang, jimbo la Java Mashariki, Oktoba 5 2022. (Picha na Ikulu ya Indonesia/Handout via Reuters)

Msemaji wa chama cha mpira wa miguu cha Indonesia anasema baadhi ya milango ya kuingia katika uwanja ambapo watu 131 walifariki dunia wiki iliyopita katika msongamano ilikuwa imefungwa wakati mchezo ulipo malizika.

Erwin Tobing, mwenyekiti wa tume ya nidhamu ya chama hicho amewaambia wanahabari Jumatano milango yote ya uwanja wa Kanjuruhan katika mji wa mashariki wa East Java wa Malang ilipaswa kuwa wazi.

Amesema utaratibu unataka milango iwe imefunguliwa dakika 10 kabla ya kumalizika mchezo wa Jumamosi baina ya wenyeji Arema FC, na Persebaya Surabaya.

Lakini Tobing amesema milango ilikuwa bado imefungwa kwa sababu maafisa walikuwa hawajafika katika milango wakati ghasia zinaanza.

XS
SM
MD
LG