Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:27

Mgogoro wa kisiasa wa Myanmar unajadiliwa na muungano wa mataifa


shambulizi la kombora la angani lililotekelezwa na jeshi la Myanmar
shambulizi la kombora la angani lililotekelezwa na jeshi la Myanmar

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia wamekutana mjini Jakarta, Indonesia, kujadiliana kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Myanmar.

Uongozi wa kijeshi wa Myanmar haujatuma mwakilishi kwenye mkutano huo ambao umefanyika kabla ya kikao cha viongozi wa ASEAN.

Myanmar imekuwa katika hali ya mgogoro tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi Februari mwaka uliopita.

Zaidi ya watu 2000 waliuawa katika msako mkali wa kijeshi dhidi ya watu wanaopinga utawala huo.

Muungano wa mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, umesema kwamba una wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuongezeka kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, lakini juhudi zake za kutatua mgogoro huo hazijafanikiwa.

Mkutano wa leo umeangazia hoja tano zilizojadiliwa April mwaka uliopita katika kikao cha dharura mjini Jakarta.

Retno Marsudi ni waziri wa mambo ya nje wa Indonesia.

"Mawaziri wa mambo ya nje wameeleza wasiwasi na kughadhabishwa kwamba hakuna hatua zimepigwa katika kutekeleza makubaliano ya hoja tano. Wasiwasi wetu ni wa wazi na baadhi ya nchi zimeeleza kukasirishwa na ukosefu wa maendeleo."

Majenerali wa jeshi la Myanmar wamepigwa marufuku kuhudhuria kikao cha juu cha mikutano ya ASEAN tangu mwaka uliopita, jeshi la nchi hiyo lilipopindua serikali ya mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Aung San Suu Kyi.

Walimfunga gerezani pamoja na wanaharakati wengine na kuanza msako mkali ambao umepelelea makundi yenye silaha kuundwa kujibu msako huo.

XS
SM
MD
LG