Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 05:55

WHO yatoa mikakati mipya ya kupambana na Ebola DRC

FILE - Madaktari na wafanyakazi wa afya wakiandamana Mashariki ya Congo, mjini Butembo on April 24, 2019, kulaani kuuawa kwa Daktari kutoka Cameroon kuuawa akiwa anatumikia Shirika la Afya Duniani kupambana na Ebola.

Wataalam wa Shirika la Afya Duniani, WHO, wametoa mwelekeo mpya wa kutoa chanjo katika juhudi za kupambana na mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Mikakati hiyo mipya ni pamoja na kuhakikisha kwamba chanjo inatolewa kwa haraka kwa kuzingatia kiwango cha dawa kinachotolewa kulingana na mahitaji.

Wataalam pia wamependekeza kuongeza idadi ya watu wanaostahili kupewa chanjo ya Ebola, kuanzisha matumizi ya dawa nyingine kwa majaribio na kuongeza idadi ya manesi, madaktari na wanafunzi wa matibabu wanaopokea mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo katika jamii zilizoathirika.

Jumla ya watu 111,000 wamepokea chanjo ya Ebola nchini DRC tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea mwaka uliopita 2018.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG