Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:19

Wizara yasema hakuna mlipuko wa Ebola Uganda


Wafanyakazi wa afya wakiwa katika kituo cha kuwasaidia walioambukizwa virusi vya Ebola, Beni, DRC.
Wafanyakazi wa afya wakiwa katika kituo cha kuwasaidia walioambukizwa virusi vya Ebola, Beni, DRC.

Wizara ya Afya nchini Uganda imesema hakuna tukio la mgonjwa wa Ebola lililo thibitishwa nchini pamoja na kuwepo taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani kuwa kuna mgonjwa amethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola katika Kijiji cha Kasenyi, karibu na fukwe za Ziwa Albert katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jimbo la Ituri.

“Mgonjwa huyo alifariki Septemba 19, 2018, katika Hospitali Kuu ya Tchomia ambayo iko karibu na Uganda. Mwanamke huyo aligusana na wagonjwa wawili (mama na dada yake) waliokuwa wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo, na hivyo ni hatarishi.

Tumepewa taarifa mgonjwa huyu alikuwa hayuko tena katika himaya ya wafuatiliaji baada ya kuhamia eneo la Kasenyi,” amesema Dkt Charles Olaro katika tamko lake.

Dkt Olaro, Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya amesema mgonjwa huyu baadae alianza kuugua, na kulazwa katika Hospitali Kuu ya Tchomia ambako baadae alifariki.

“Alichukuliwa vipimo na matokeo yaliyo tolewa Septemba 21, 2018 yalithibitisha kuwa alikuwa na virusi vya Ebola. Timu ya wataalamu kutoka Beni imefika tayari katika eneo hilo kufanya uchunguzi wa mgonjwa huyu aliyekufa, kumtambua na kupata taarifa za watu ambao aliwahi kugusana nao kwa ajili ya kuwafuatilia na kuchukua hatua zinazo hitajika kukabiliana na hali hiyo,” amesema Dr Olaro.

Ameongeza kuwa: “Tunafahamu ya kuwa kuna idadi kubwa ya watu ambao wanasafiri kuvuka Ziwa Albert kuja Uganda na kuwa hali hiyo ni hatarishi sana juu ya kueneza maradhi hayo nchini Uganda. Wizara ya Afya na Washirika wake wanaendelea kusaidia wilaya zote zinazo pakana na DRC ili kuongeza maandalizi na utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unaoweza kujitokeza nchini Uganda.”

XS
SM
MD
LG