Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:12

Waziri wa Fedha awasilisha bajeti ya serikali ya awamu ya sita


Dkt Mwigulu Nchemba
Dkt Mwigulu Nchemba

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amewasilisha bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya sita bungeni.

Bajeti hiyo iliyosomwa jijini Dodoma, Alhamisi imeomba kiasi cha shilingi trilioni 36.3 ziidhinishwe kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo ya serikali.

Bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2021/22 imetanguliwa uwasilishaji wake na hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka unaomalizika na Mpango wa Taifa wa maendeleo wa Mwaka ujao 2021/2022.

Akiwasilisha bajeti hiyo Dkt Nchemba amebainisha kwamba katika makadirio ya bajeti hii ya zaidi ya shilingi trilioni 36.3, matumizi ya kawaida ni takribani shilingi trilioni 23 wakati matumizi ya mendeleo ni takribani shilingi trilioni 13.3

Serikali pia katika bajeti hii imesema itaendelea kuimarisha makusanyo ya kodi hata hivyo ikiondoa kodi ambazo zinaonekana ni kero

Katika kuondoa kero kwa wananchi hasa wa kipato cha chini serikali katika bajeti hii ya 2021/22 imependekeza kupunguza adhabu ya makosa ya barabarani kwa waendesha bajaji na pikipiki kutoka shilingi elfu 30 kwa kosa moja hadi shilingi 10,000 kwa kosa.

Aidha serikali imependekeza kuanza kutolewa kwa posho ya kila mwezi kwa madiwani na kulipwa moja kwa moja kwenye akaunti zao huku pia maafisa tarafa ikipendekezwa kulipwa shilingi laki moja kwa mwezi na watendaji wa kata shilingi laki moja pia kwa mwezi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mpiango bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 pia inatoa kipaumbele katika maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, inayotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 328.2.

XS
SM
MD
LG