Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 10:49

Ripoti ya CAG yaibua mijadala Zanzibar


Rais Hussein Mwinyi
Rais Hussein Mwinyi

Wananchi visiwani Zanzibar wamekuwa na maoni tofauti baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyotolewa Jumapili kuonyesha kasoro katika matumizi na ubadhirifu wa fedha za umma.

Ripoti inaonyesha mapungufu hayo katika sekta mbalimbali za serikali, baadhi wakieleza kuwa ripoti hiyo ni kipimo kwa Rais Hussein Mwinyi katika usimamizi wa fedha za umma na nidhamu ya matumizi serikalini.

Tangu kutoka kwa ripoti ya CAG huko Zanzibar na kubainisha upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 5 fedha za Tanzania ambazo hazijulikani zilipo mijadala mingi imeibuka hasa juu ya usimamizi wa fedha za umma.

Baadhi ya taasisi na wizara ikiwemo ya Kilimo pamoja na Jeshi la Magereza ni miongoni mwa maeneo yaliyonyooshewa kidole katika ripoti hiyo huku tabia za baadhi ya taasisi kutotoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG ikionekana kuendelea kuota mizizi.

Katika mitaa ya Unguja visiwani Zanzibar ripoti hii imeibua maoni tofauti, kuna baadhi wakiamini hii itakua kipimo kwa Rais Mwinyi katika usimamizi wa fedha za umma na nidhamu katika matumizi ya Serikali

Lakini wengine wanataka serikali iwe na mkono mrefu kuwafikia wanaofuja fedha za umma kwani ubadhirifu unaofanywa unakwamisha pakubwa utolewaji wa huduma muhimu kwa jamii

Hata hivyo Rais Hussein Mwinyi ameeleza kuwa atachukua hatua kwa yote yaliyoibuliwa katika ripoti hii na kusisitiza kuwa ili kuyafikia malengo katika kujenga uchumi wa bluu uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa fedha za umma ndio msingi utakofanikisha hilo

Aidha Rais Mwinyi ameagiza mashirika na taasisi zote ambazo hazikukaguliwa na CAG kwa kushindwa kutoa ushirikiano, CAG aende kuzikagua mapema iwezekanavyo na kuwasilisha ripoti zao.

XS
SM
MD
LG