Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:13

Tanzania yaruhusu uagizaji wa chanjo ya COVID-19


Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania

Tanzania imesema Ijumaa ofisi za ubalozi na mashirika ya kimataifa yanaweza kuagiza chanjo ya COVID-19 kuchanja raia na wafanyakazi dhidi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Reuters hatua hiyo ni sehemu ya hatua za mapema kukabiliana na ugonjwa huo ambapo kwa muda mrefu serikali ya Tanzania ilikuwa haijakiri kwamba kuwa janga la Covid 19 limeingia nchini humo.

Tangazo hilo la serikali limekuja baada ya wataalam kuwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan mpango unaojumuisha utoaji wa chanjo nchini.

“Rais Samia (Suluhu Hassan) amesema ofisi za ubalozi na jumuiya za kimataifa zimeruhusiwa kuingiza chanjo ya COVID-19 kuwachanja wananchi wao na wafanyakazi ili kukidhi matakwa ya nchi zao na matakwa ya taasisi na kuondoa vikwazo katika shughuli zao za kila siku,” taarifa ya ofisi ya rais imesema.

Wizara ya Afya itaendelea kuratibu uagizaji wa chanjo hizo kwa ajili yao, imeongeza.

Tanzania ni moja ya nchi chache za Kiafrika ambazo bado hazijapokea chanjo, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Serikali imeripoti maambukizi 509 na vifo 21 vinavyotokana na COVID-19 kabla haijasitisha kuripoti maambukizi mwezi Mei 2020.

Wataalam wameshauri serikali kuanza kuchapisha takwimu sahihi.

XS
SM
MD
LG