Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 11:07

Tanzania : Rais Samia ni Mwenyekiti mpya wa CCM


Mwenyekiti wa CCM mpya Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhiwa na Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama chake Chama cha Mapinduzi CCM kuwa Mwenyekiti wa sita wa Chama hicho.

Rais Samia alipigiwa kura 1862 sawa na asilimia 100 ya kura zilizopigwa kumuidhinisha katika Mkutano huo Maalum uliofanyika Dodoma.

Katika hotuba yake Rais Samia ambaye amekuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 34, miaka 20 ya uongozi ndani ya chama umempa uzoefu wa kutosha.

Uzoefu huo ni katika ushiriki wake ndani ya vikao vikubwa vya kufanya maamuzi katika uongozi wa chama.

Pia Mwenyekiti Samia ameahidi uongozi unaozingatia katiba na misingi ya CCM.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CCM Samia amemteua Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa chama hiko, Chongolo alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG