Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 16:22

Tanzania na Uganda zasaini mikataba ya sekta ya mafuta na gesi


Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni, Kampala, Uganda.

Tanzania na Uganda zimesaini mikataba katika maeneo matatu muhimu ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi ya Uganda.

Mikataba hiyo imesainiwa wakati wa ziara ya kwanza ya nje ya nchi ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Utiaji saini huo umefanyika kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) kwenda Tanga (Tanzania).

Makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki yamejikita katika masuala ya hisa, usafirishaji na ushuru.

Mradi huu una manufaa makubwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wa jumla ya Kilometa 1,443 kutoka magharibi mwa Uganda hadi kwenye bandari ya Tanga katika bahari ya Hindi, Tanga.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG