Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:16

Benki ya Dunia yaidhinisha mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania


Mwigulu Nchemba -Michuzi blog
Mwigulu Nchemba -Michuzi blog

Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania.

Mikopo hiyo yenye thamani ya Shilingi trilioni 2.3 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo, kwa mujibu wa Waziri wa fedha wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Mwigulu Nchemba.

Nchemba amesema kati ya miradi iliyopatiwa fedha hizo, ni ya uboreshaji wa barabara za vijijini, na ule wa kuimarisha mazingira na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu.

Mradi mwengine ni ule wa kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za mtandao, maarufu DTP, na wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora, na za uhakika za Umeme visiwani Zanzibar, Zesta.

Dkt Nchemba alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Jumapili, siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake ya mwaka wa fedha 2021/2022.

XS
SM
MD
LG