Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 23:17

Waziri Mkuu Modi apongeza mafanikio ya chanjo


India yaweka rekodi ya mafanikio ya chanjo
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:13 0:00

India yaweka rekodi ya mafanikio ya chanjo.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amepongeza siku ya kihistoria Alhamisi wakati nchi yake imefikia hatua muhimu ya kutoa dozi bilioni moja ya chanjo ya COVID-19 wakati ambapo kirusi cha delta kilichochea kuongezeka kwa maambukizi mapema mwaka 2021.

Bendera ya India ilipeperushwa katika sherehe hizo kwenye eneo la kihistoria la Red Fort mjini New Delhi.

Takriban asilimia 75 ya watu wazima nchini india wamepata chanjo hiyo angalau dozi moja wakati asilimia 30 wamechanjwa dozi kamili.

Nchi yenye takriban watu bilioni 1.4 ni ya pili kuvuka kipimo cha chanjo bilioni moja baada ya taifa maarufu la China kufanya hivyo mwezi Juni.

Maambukizi ya virusi vya corona yameshuka kwa kiwango kikubwa tangu miezi ya kutaabika mwanzoni mwa mwaka huu wakati kulikuwa na maambukizo ya juu ya kirusi hicho cha delta.

Kirusi hicho kilichogundulika kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka mmoja uliopita na kuathiri maelfu ya watu, kikisababisha wagonjwa kulazwa hospitali na kujaza maeneo ya kuchomea miili ya watu waliokufa.

“ Tarehe 21 mwezi Octoba mwaka 2021, imekuwa siku ya kihistoria. Muda mchache uliopita India imevunja rekodi kwa kutoa chanjo ya bilioni moja kupambana na janga kubwa zaidi katika miaka mia moja, nchi ina ngao ya kinga ya bilioni moja,” amesema Waziri Mkuu.

XS
SM
MD
LG