Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:50

Kesi za virusi vya Zika zimethibitishwa kuwepo India


Mfano wa mbu aina ya Aedes anayesabaisha kirusi cha Zika
Mfano wa mbu aina ya Aedes anayesabaisha kirusi cha Zika

Kesi nyingine 13 zinazoshukiwa zilikuwa zikichunguzwa waziri wa afya wa jimbo, Veena George alisema. Virusi vya Zika viligundulika kwa mara ya kwanza kwa nyani katika msitu wa Zika nchini Uganda mwaka 1947 na imesababisha milipuko kadhaa duniani katika miongo ya karibuni.

Mamlaka katika mkoa wa kusini wa Kerala nchini India wametoa tahadhari ya jimbo zima baada ya kesi za virusi vya Zika kuthibitishwa maafisa walisema Ijumaa.

Kesi nyingine 13 zinazoshukiwa zilikuwa zikichunguzwa waziri wa afya wa jimbo Veena George alisema. Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 24 aligundulika ameambukizwa ugonjwa unaosababishwa na mbu, na alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali kwenye mji wa Thiruvananthapuram.

Wanawake wajawazito wapo hatarini na wanaweza kusambaza maambukizi kwa watoto wao wachanga, jambo ambalo linaweza kupelekea hali ya maradhi ya kudumu, kama vile ugonjwa wa Guillain-Barre, ugonjwa nadra wa kinga ya mwili.

Sampuli za kesi 13 zinazoshukiwa, zimetumwa kufanyiwa uchunguzi zaidi kwenye maabara huko Pune, waziri huyo aliongeza. Zika husambaa haraka kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes, lakini pia unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono, kulingana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Marekani.

Virusi viligundulika kwa mara ya kwanza kwa nyani, katika msitu wa Zika nchini Uganda mwaka 1947 na imesababisha milipuko kadhaa duniani katika miongo ya karibuni. Hakuna chanjo au dawa zilizopo za kuzuia virusi kama kinga au tiba.

XS
SM
MD
LG