Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:45

COVID-19 : Wito waongezeka kumtaka Modi kufunga shughuli nchini India


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Wito umeendelea kuongezeka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, kufunga shughuli katika nchi yake, ambayo ni ya pili kwa wingi wa watu duniani, huku maambukizi virusi vya Corona, na vifo vilivyotokana na ugonjwa wa COVID-19, vikiripotiwa kuongezeka, nusra vivunje rekodi Jumatatu. 

Maambukizi mapya 366,161 na vifo 3,754 vilivyoripotiwa na Wizara ya Afya, ikipandisha idadi ya maambukizi nchini India hadi milioni 22.66 na vifo 246,116 wakati hospitali nyingi zimepungukiwa na oksijeni na vitanda, na kufurika kwa vyumba vya kuhifadhia maiti.

Majimbo mengi yameweka vikwazo vikali zaidi katika mwezi uliopita, wakati wengine wameweka zuio la shughuli mbalimbali na kufunga kumbi za sinema, migahawa, baa na maduka makubwa.

Lakini shinikizo linazidi kuongezeka kwa Modi kutangaza kufungwa kwa nchi nzima kama alivyofanya wakati wa wimbi la kwanza la maambukizo mwaka 2020.

Anapambana na ukosoaji kwa kuruhusu mikusanyiko mikubwa kwenye sherehe za kidini na kufanya mikutano mikubwa ya uchaguzi, katika miezi miwili iliyopita hata wakati visa vya maambukizi, vilikuwa vikiongezeka.

XS
SM
MD
LG