Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 12:43

India yaripoti maambukizi mapya 300,000 ya COVID-19


Watu wenye tatizo la kupumua wakipokea huduma ya msaada wa oxygen nje ya eneo la kuabudu Gurudwara (Sikh temple), wakati kuna ongezeko la maambukizi ya COVID-19, huko Ghaziabad, India, Aprili 30, 2021.

India imeripoti zaidi ya kesi mpya 300,000 za COVID-19 kila siku kwa siku 12 mfululizo.

Siku ya Jumatatu taifa hilo la Asia Kusini limeripoti kesi 368,147 katika saa 24 zilizopita.

Wakati India ina moja ya makampuni makubwa ya kutengeneza chanjo duniani, Serum Institute of India, asilimia 2 pekee ya watu billioni 1.3 ndio wamekwisha pewa chanjo, kwa mujibu wa ripoti za ndani.

Mkuu wa utawala kwenye ofisi ya Rais Joe Biden, Ron Klain ameiambia televisheni ya CBS Marekani imeanza kupeleka msaada India.

Hata hivyo, Marekani pia imechukua hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi. Kuanzia Jumanne, hakuna ndege zitaingia Marekani kutoka India.

Marekani ilipeleka nchini India vifaa tofauti vya kupambana na janga la COVID-19, ikiwemo mitungi ya oxygen, barakoa na vifaa vya kufanya vipimo vya COVID-19 kwa haraka. Nchi kadhaa za dunia pia zilituma msaada nchini India.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG