Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:15

Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka kwa kasi India


Watu wakisubiri kuchoma moto miili ya waliokufa kutokana na janga la corona katika eneo la Wahindu la kuchomea maitiNew Delhi, India, April 23, 2021. REUTERS/Danish Siddiqui

Maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini India yanaongezeka kwa kasi ya kutisha.

Wizara ya afya ya nchi hiyo Ijumaa imesema imehesabu rekodi ya maambukizi mapya zaidi ya 330,000 katika saa 24 zilizopita. Idadi hiyo mpya inavuka rekodi ya Alhamisi ya maambukizi mapya ya kila siku ambayo yalikuwa zaidi ya 310,000.

Hospitali 6 za mji mkuu New Dehli zinakabiliwa na uhaba wa matenki ya oksijeni kwa wagonjwa wao.

Moto ambao umetokea leo kwenye hospitali ya Vijay Vallabh magharibi mwa India umeua wagonjwa 13 wa covid 19.

Waziri Mkuu Narendra Modi amefanya mikutano na mawaziri viongozi wa nchi ili kubuni njia bora ya kukabiliana na janga hilo.

Chuo kikuu cha John Hokpins hapa Marekani kimeripoti kuwa India imevuka kesi mpya millioni 16 za covid 19.

Marekani ni nchi pekee ambayo ina kesi millioni 32 ikiizidi India.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG