Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:46

Umoja wa Afrika wachunguza chanjo ya Johnson & Johnson


John Nkengasong
John Nkengasong

Umoja wa Afrika umeacha mipango ya kununua chanjo za COVID-19 kutoka Taasisi ya Serum ya India kwa ajili ya mataifa ya Afrika na inachunguza juu ya chanjo ya Johnson & Johnson, mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, CDC, Afrika alisema Alhamisi. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters taasisi hiyo bado itasambaza chanjo ya AstraZeneca Afrika kupitia kituo cha ushirikiano wa chanjo cha COVAX, mkuu huyo wa CDC Afrika, John Nkengasong aliwaambia waandishi wa habari, lakini Umoja wa Afrika utaagiza chanjo zaidi kutoka kwa Johnson & Johnson.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya wasimamizi wa dawa Ulaya na Uingereza kusema wamegundua uhusiano kati ya chanjo ya AstraZeneca na ripoti za visa adimu vya kuganda kwa damu kwenye ubongo, lakini walisisitiza umuhimu wake katika kulinda watu.

Nkengasong alisema uhusiano huo wa watu kuugua hauhusiani na uamuzi wa Umoja wa Afrika.

Kundi hilo la nchi wanachama 55 lilibadilisha juhudi zake na kuzielekeza kwenye chanjo ya Johnson & Johnson, alisema, akinukuu mpango uliotiwa saini wiki iliyopita kupata hadi dozi milioni 400 kuanzia robo ya tatu ya mwaka huu.

XS
SM
MD
LG