Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 04, 2023 Local time: 05:37

Kenyatta atangaza amri mpya kudhibiti COVID-19 Kenya


Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta, katika hotuba yake Ijumaa mchana, ameeleza Kenya imeripoti ongezeko la maambukizi ya Covid-19. Kiwango hiki ni cha juu zaidi kuliko wakati janga hilo lilipoanza.

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya

Ameamuru kusitishwa vikao vya kawaida vya bunge la Agosti, na mabunge ya kwenye kaunti za Nairobi, Machakos, Kajiado, Kiambu na Nakuru na kamati zake zote.Katazo la kutoka nje usiku

Muda wa kutotoka nje usiku nchi nzima umerekebishwa kwa maeneo husika ikiwemo Kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado na Nakuru, na sasa amri hiyo itaanza kutekelezwa saa mbili usiku hadi saa kumi Alfajiri.

Amri ya kutotoka nje usiku maeneo mengine nchi nzima itakuwa kama ilivyokuwa awali, na hivyo ni kuanzia saa nne usiku.

Wanafunzi kutohudhuria madarasani

Rais Kenyatta ameamrisha kusitishwa mahudhurio ya wanafunzi madarasani katika vyuo vyote ikiwemo vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya ufundi. Ila tu kwa wale wanaofanya mitihani ya mwisho ya kumaliza masomo na wale katika vyuo vya afya hadi tamko litakapotolewa.

Kusitishwa Michezo

Shughuli zote za michezo zimesitishwa ikiwemo ile inayoendeshwa na wanachama wa vilabu hivyo.

Katazo la Mabaa na Uuzaji wa Pombe

Kenyatta pia ametoa amri ya kusitishwa biashara za kwenye baa katika kaunti 5 zilizoathiriwa zaidi na Covid-19 kuanzia saa sita usiku. Pia sitisho hilo la biashara za mabaa litatekelezwa Nairobi,

Shughuli za Kwenye Migahawa

Kadhalika uuzaji wa Pombe katika maeneo ya migahawa katika kaunti tano umepigwa marufuku. Na pia migahawa katika maeneo hayo hivi sasa yatauza vyakula na wateja watakiwa kuvichukua majumbani na siyo kula ndani ya migahawa.

Migahawa katika maeneo mengine ya nchi itaendelea kutoa huduma kama kawaida kwa kufuata miongozo ya afya ya umma.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG