Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 17, 2022 Local time: 11:35

COVID-19 : Kenya yawazuia wanariadha wake kushiriki mashindano Tanzania


Ramani ikionyesha eneo la Kenya na Tanzania

Kenya imekataa kutoa idhini kwa wanariadha wake kushiriki kwenye mbio za marathon za Kilimanjaro nchini Tanzania kutokana na wasi wasi wa janga la ugonjwa wa Covid 19.

Mashindano hayo yanayo tambuliwa na shirikisho la kimataifa la riadha, IAAF, yatafanyika Jumapili asubuhi kwenye Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi Afrika.

Katika taarifa yake shirika la riadha la Kenya limewahimiza wanariadha wote wasisafiri hadi Tanzania kushiriki kwenye mashindano hayo.

Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakishinda kwenye mashindano yaliyopita.

Shirika la Afya Duniani mapema wiki hii lilIihimiza Tanzania kuanza kuripoti watu wanao ambukizwa virusi vya corona na kulipatia shirika hilo takwimu za maambukizi mayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG