Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:28

Fauci asema Marekani iko katika mwelekeo sahihi wa kudhibiti COVID-19


Dkt Anthony Fauci
Dkt Anthony Fauci

Mtaalam wa juu wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani alisema Jumapili nchi hiyo iko katika mwelekeo sahihi na mamilioni ya Wamarekani wanapokea chanjo ya Corona, lakini alikuwa mwangalifu juu ya idadi kubwa ya maambukizi iilivyo.

Akiongea kwenye kipindi cha NBC-TV Meet the Press, Anthony Fauci alionya kwamba unapopata wagonjwa wapya katika kiwango karibu na maambukizo mapya 60,000 kwa siku, kila wakati kuna hatari ya kuongezeka tena.

Fauci alitumia Italia kama mfano wa eneo ambalo kesi zilipungua. Alisema Italia walipoona wanaingia kwenya idadi ya kupungua kwa kesi wakaacha kuchukua hatua za kiafya za umma, ambapo ilichangia kuongezeka kwa maambukizi ya sasa kwa nchi hiyo.

Hali hiyo imewalazimisha maafisa kuweka sehemu ya nchi hiyo kwenye karantini Jumatatu. Aliwasihi watu kuendelea kuheshimu hatua za kiafya za umma, hasaa kuvaa barakoa.

Marekani inabaki inashikilia idadi ya juu katika orodha ya kesi za COVID-19, kulingana na Kituo cha Johns Hopkins, chombo cha utafiti kinachotoa kila wakati idadi ya COVID-19 na uchambuzi wa kitaalam.

Marekani ina maambukizi milioni 29.4 ya maambukizi duniani ya karibu milioni 120 ya COVID-19 ikifuatiwa na Brazil yenye milioni 11.4 na India milioni 11.3.

Wakati huo huo kampuni ya AstraZeneca ilisema Jumapili kwamba utafiti wa mapitio ya taarifa zake haukuonyesha kuwa chanjo yao inasababisha kuganda kwa damu.

XS
SM
MD
LG