Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:22

Waziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani waanza ziara Japan na Korea Kusini


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, na waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, Jumatatu, wanaanza ziara ya siku nne ya Japan, na Korea Kusini.

Ziara hiyo ni kwa ajili ya kuonyesha ushirikiano na mataifa hayo mawili yenye ushirika na Marekani.

Ziara hii inakuja ikiwa inaonekana kuwa suala la vitisho vya China, na Korea Kaskazini, kuwa ndivyo vitakavyo gubika safari ya kwanza ya mawaziri wa utawala wa rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden.

Ni sehemu ya juhudi kubwa za kuongeza ushawishi wa Marekani, na kupunguza wasiwasi kuhusu nafasi ya Marekani katika bara la Asia.

Afisa wa juu wa Marekani, anasema kwamba Marekani, ilijitahidi kuwasiliana na Korea Kaskazini, lakini mpaka sasa haijajibiwa.

Kutokana na hilo imefanya kuwa ni muhimu kwa Marekani, kukutana na mataifa jirani na Korea Kaskazini, ya Japan, Korea Kusini, na China, na kuwa ni jambo muhimu.

XS
SM
MD
LG