Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 23:19

Makamu wa rais wa Marekani na mkuu wa WTO waahidi kufanyakazi pamoja


Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris

Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris, na mkurugenzi wa shirika la biashara la dunia (WTO), Alhamisi wamekubaliana kuhusu mahitaji ya kufanyiwa mabadiliko ya biashara za dunia, na kuahidi kufanyakazi pamoja kuongeza kasi ya uchumi wa dunia.

Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya Marekani, Harris ambaye ni makamu wa rais wa kwanza mwanamke mweusi na mwenye asili ya Asia, na ameahidi kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi wa WTO, Dr Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye ni mwafika na mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi hiyo yenye makao yake makuu Geneva.

Mazungumzo yao yamefanyika Alhamisi kwa njia ya simu kwa mujibu wa White House.

Viongozi hao wawili pia wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kuboresha biashara na kuleta usawa, na ukuwaji wa uchumi, pamoja na jukumu ambalo litaboresha hali ya maisha, hali za kazi, haki za binadamu, na ustawi wa familia za wafanyakazi wanaoweza kuwa na jukumu la kutunga sera.

Kwa pamoja wamekubaliana kufanyakazi kushughulikia athari za Covid-19 katika uchumi na afya pamoja na mabadiliko ya tabia nchi huku ikihakikishwa dunia inaendelea na hali yake ya kawaida.

Makamu wa rais Harris amezungumzia pia vipaumbele vya Marekani katika kuwekeza katika afya na teknolojia ikiwa ndio ukuwaji uchumi na kukuza maendeleo endelevu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG