Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:53

COVID-19 : Uingereza kupiga marufuku wasafiri kutoka Kenya


Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Serikali ya Uingereza, kuanzia Ijumaa wiki ijayo, itapiga marufuku wasafiri kutoka Kenya, kuingia nchini humo, kama njia ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya serikali GOV.UK, Uingereza inasema, kuwa baadhi ya wasafiri kutoka Kenya, wamepatikana wakiwa na aina ya virusi vipya, vya ugonjwa huo, kutoka Afrika Kusini.

Kenya imekuwa nchi ya hivi karibuni kabisa, kuongezwa kwenye orodha ya nchi ambazo, wasafiri wake hawaruhusiwi kuingia Uingereza, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu aina mpya ya viurusi vya Covid-19.

Isipokuwa raia wa Uingereza na Ireland, Wasafiri ambao watakuwa wamepitia, Kenya, Ufilipino, Pakistan and Bangla-desh, siku kumi kabla ya tarehe tisa mwezi huu, hawataruhusiwa kuingia Uingereza.

XS
SM
MD
LG