Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:43

Wanadiplomasia waridhia ajenda za mkutano ujao wa Trump na Kim


Mwakilishi maalum wa Marekani huko Korea Kaskazini Stephen Biegun, kushoto, akifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Korea Kusini Chung Eui-yong Seoul, South Korea, Feb. 4, 2019.
Mwakilishi maalum wa Marekani huko Korea Kaskazini Stephen Biegun, kushoto, akifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Korea Kusini Chung Eui-yong Seoul, South Korea, Feb. 4, 2019.

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Marekani katika mazungumzo ya Korea Kaskazini amerejea kutoka Pyongyang ambako alihudhuria kikao cha siku tatu na atakutana tena na mwenzake wa upande wa Korea Kaskazini kabla ya mkutano wa pili kati ya Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Jumamosi kuwa viongozi hao watakutana huko mji mkuu wa Vietnam, Hanoi baadae mwezi Februari 2019.

Stephen Biegun atoa muhtasari

Stephen Biegun, Mwakilishi maalum wa Marekani, Korea Kaskazini, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Kang Kyung-wha na mjumbe ambaye ni mkuu wa programu ya nyuklia Seoul, Lee Do-hoon, Jumamosi kuwapa muhtasari wa mazungumzo yake aliyofanya na Korea Kaskazini.

“Mazungumzo yetu yalikuwa na tija,” Biegun amesema wakati akikutana na Kang. “Rais anajitayarisha kuchukua hatua nyingine. Tuna kazi ngumu ya kutekeleza na serikali ya Korea Kaskazini kati ya sasa na hapo mkutano utakapofanyika. Lakini ninaamini kuwa pande zote mbili iwapo tutaweza kuendeleza msimamo huu, tutaweza kupiga hatua za uhakika,” amesema.

Shinikizo la kuondoa kabisa silaha za nyuklia

Kang wa Korea Kusini alikuwa na maoni chanya kuhusu habari alizotoa Biegun huko Pyongyang.

“Bila shaka tunakuunga mkono kikamilifu wakati ukiendelea na matayarisho ya mkutano huo wa marais na hata baadaye,” waziri wa mambo ya nje amesema.

Huko Pyongyang, Biegun na Kim Hyok Chol, mjumbe maalum wa Korea Kaskazini katika kushughulikia masuala ya Marekani, walijadili “kuendeleza makubaliano ya mkutano wa Trump na Kim uliofanyika Singapore juu ya kuondoa kabisa silaha za nyuklia, kuboresha mahusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini na kujenga amani ya kudumu katika Rasi ya Korea,” Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika tamko lake.

Tamko hilo limesema kuwa Biegun na Kim walikubaliana kukutana tena kabla ya viongozi hao kukutana mara ya pili katika kikao kilichopangwa kufanyika Februari 27-28 huko Hanoi, Vietnam.

Trump atuma ujumbe wa tweet

Trump alituma ujumbe wa Tweet Ijumaa akiwa Washington kueleza pale mkutano utakapofanyika, akisema kuwa Biegun tayari alikuwa ameshaondoka North Korea baada ya “mazungumzo yenye mafanikio” juu ya mkutano wa Hanoi.

Trump ameongeza kuwa : “Natarajia kukutana na Mwenyekiti Kim na kutanguliza kuwepo muelekeo wa amani!”

Hapo awali rais alikuwa ametangaza kuwa mkutano wake na Kim utafanyika Vietnam, lakini jiji la Hanoi lilikuwa halikutaarifiwa.

Wataalam watahadharisha

Watalaam wa nyuklia nchi za magharibi kwa mujibu wa vyanzo vya habari wanasema suala la Korea Kaskazini kuhusu silaha za nyuklia linapaswa kuangaliwa kwa uzito na kupatiwa ufumbuzi wa kina wakati viongozi hao wawili watakapokutana.

XS
SM
MD
LG