Korea kaskazini imesema kwamba haitaacha mpango wake wa kutengeneza silaha za nuclear kwa kubadilisha na tangazo rasmi la kumaliza vita vya Korea.
Taarifa kupitia kwa shirika la habari la korea kaskazini inasema kwamba makubaliano rasmi ya Amani yanaweza kuwa fursa nzuri ya majadiliano yatakayoifanya korea kaskazini kuacha kutengeneza silaha za nuclear.
wazo la kusaini makubaliano rasmi ya Amani limeangaziwa sana wakati wa mkutano wa hivi karibuni kati ya Pyongyang, Seoul na Washington, yenye lengo la kumaliza utengenezaji wa silaha za nuclear katika Pennisula ya Korea.