Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:15

Wanajeshi wa Korea Kusini, Kaskazini watembeleana

Viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini walipokutana Seoul, Korea Kusini, Octoba 23, 2018. Rais wa Korea Kusinit Moon Jae-in, wapili kulia, mkewe Kim Jung-sook, kulia, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Mkewe.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevuka mpaka na kuingia Korea kusini, sawa na wale wa Korea kusini walioingia Korea kaskazini katika hali ya amani na maridhiano, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1950.

Wanajeshi hao wameanza shughuli ya kuondoa silaha katika vituo vya ulinzi mpakani, katika sehemu isiyo na shughuli za kijeshi.

Korea kaskazini ilishambulia upande wa kusini mwaka 1950 na kusababisha vita vya Korea, vilivyomalizika mwaka 1953 lakini vikaacha uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Juhudi za kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo zimekuwa zikiendelea tangu mwanzoni mwa mwaka 2018.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na mwenzake wa Kaskazini Kim Jong Un mwenye silaha za nyuklia, walikubaliana mwezi Septemba, 2018 katika mkutano wao wa Pyongyang, kupunguza idadi ya vituo vya ulinzi mpakani. Nchi zote mbili zimeharibu vituo kumi hadi sasa.

XS
SM
MD
LG