Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:46

Trump na Kim watakutana tena haraka iwezekanavyo


Kim Jong Un (L) na Rais Donald Trump
Kim Jong Un (L) na Rais Donald Trump

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong UN wamekubaliana kupanga mkutano wa awamu ya pili kati ya Marekani na Korea kaskazini haraka iwezekanavyo, ofisi ya Rais wa Korea kusini ilisema Jumapili.

Tangazo hilo lilikuja muda mfupi baada ya Pompeo alipowasili Seoul kufuatia ziara yake ya siku nne kuelekea Korea kaskazini mahala ambapo alikutana na Kim. Pompeo alisema Marekani na Korea kaskazini walikubaliana kuendeleza mazungumzo na kuchagua tarehe maalumu pamoja na mahala ambako mkutano ujao utafanyika kulingana na taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Korea kusini, Moon Jae-In.

Moon alimshukuru Pompeo kwa ziara yake na aliwatakia mafanikio mema kwenye mkutano ujao kati ya Kim na Rais Donald Trump wa Marekani. Viongozi hao wawili walikutana mara ya mwisho mwezi June mwaka 2018 huko Singapore.

XS
SM
MD
LG