Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 09:33

Wakuu wa Ulinzi wa Marekani na Russia wazungumza kwa mara ya kwanza tangu mwezi Oktoba 2022


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alizungumza na mwenzake wa Russia Jumatano kuhusu jeshi la Russia kuingilia droni ya upelelezi ya  Marekani na kusababisha  kuanguka Jumanne katika bahari ya Black Sea. 

“Marekani itaendelea kuruka na kufanya operesheni zake mahali popote sheria za kimataifa zinaporuhusu kufanya hivyo, na ni juu ya Russia kuendesha ndege zake za kijeshi kwa usalama na kwa weledi,” Austin aliwaambia waandishi wa habari baada ya kutangaza kwamba alikuwa “amemaliza kuzungumza kwa simu” na waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa mazungumzo ya simu kufanyika kati ya viongozi hao wawili wa ulinzi tangu mwezi Oktoba 2022, kulingana na maafisa.

Droni hiyo ya Marekani MQ-9 iliyotunguliwa ilikuwa “ikifanya operesheni za kawaida” katika anga ya kimataifa Jumanne, kulingana na jeshi la Marekani, ni pale ndege mbili za kivita za Russia aina ya Su-27 “zilipomwaga mafuta na kuruka mbele ya droni MQ-9.

“Tunajua kwamba uingiliaji huo ulikuwa wa makusudi. Tunafahamu kitendo hicho cha uchokozi ni cha makusudi. Pia tunafahamu kimefanyika bila weledi na si salama hata kidogo,” Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa Wakuu wa Pamoja wa Kijeshi, aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

Jenerali Mark A. Milley,
Jenerali Mark A. Milley,

Milley alisema “hakuwa na uhakika” iwapo kugusana kati ya ndege ya Russia na Droni ilikuwa ni kwa makusudi.

Milley pia alisema kuwa Marekani ina ushahidi wa video inayoonyesha kitendo cha uchokozi wa kuingilia kati.

Pia alizungumza na mwenzake wa Russia kwa simu baadae Jumatano kuhusu “masuala kadhaa yanayohusiana na usalama yanayotia wasi wasi,” kwa mujibu wa msemaji wake.

Russia ilisema inafikiria iwapo ijaribu kuirudisha droni hiyo, lakini maafisa wa Marekani walisema watendaji wake walifanikiwa kufuta programu nyeti kwa mbali katika mashine ya droni hiyo kuizuia Russia kukusanya taarifa za siri kabla ya kuipeleka droni hiyo ndani ya bahari ya Black Sea.

Marekani haina meli zozote katika bahari ya Black Sea, ambayo kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na Russia.

“Lakini tunao washirika wengi na marafiki katika eneo hilo, na tutafanya operesheni za kuifikia na kuichukua droni hiyo.

XS
SM
MD
LG