Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:10

Marekani yaelezea wasiwasi kuhusu "teknolojia ya China kutumika barani Afrika"


Mkutano kati ya Rais Xi Jing Ping na baadhi ya mawaziri wa nchi za Afrika.
Mkutano kati ya Rais Xi Jing Ping na baadhi ya mawaziri wa nchi za Afrika.

Marekani imeendelea kuelezea wasiwasi wake kuhusu hatari ya nchi za Kiafrika kutumia teknolojia ya China, na  ufuatiliaji wa mawasiliano ya simu, ambao inasema unafanywa na nchi hiyo barani Afrika.

Kundi la wabunge wa Marekani hivi karibuni liliandaa rasimu ya azimio la kukosoa serikali ya Afrika Kusini kwa uhusiano wake wa karibu na Beijing, ikiwa ni pamoja na matumizi yake ya teknolojia ya China, na kumtaka Rais Joe Biden kuufanyia tathmini uhusiano wa Marekani na Pretoria.

Hata hivyo, wachambuzi wengine wanasema ni wajibu wa kila serikali kutumia teknolojia kwa uwajibikaji, na China sio mdau pekee katika sekata ya teknolojia.

Azimio hilo liliwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi la Marekani wakati Afrika Kusini ikifanya mazoezi ya majini na China na Russia mwezi Februari.

Marekani tayari imepiga marufuku matumiai ya vifaa vya kampuni ya teknolojia ya China, Huawei, ikisema ni hatari kwa usalama wa taifa. Pia kuna msukumo kwenye bunge kupiga marufuku programu ya mtandao wa kijamii ya China, TikTok.

Barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo chini ya asilimia 30 ya watu wanatumia internet, serikali nyingi zinakaribisha uwekezaji wa China katika miundombinu ya kidijitali - sehemu ya Mpango wa uitwao Belt and Road, ambao pia umekuja kujulikana kama Digital Silk Road, yani barabara ya hariri ya kidijitali.

Kwa sababu ya ruzuku ya serikali ya China, nchi hizo zinaichukulia kama njia nafuu ya kuunganishwa zaidi.

XS
SM
MD
LG