Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:43

ANC yapuuzia ukosoaji wa kupokea ufadhili wa tajiri wa Russia


Rais wa African National Congress-ANC Cyril Ramaphosa akitoa salamu za Black Power mwishoni mwa Kongamano la Kitaifa la 55 huko Johannesburg, Afrika Kusini, Jumanne, Desemba 20, 2022.AP
Rais wa African National Congress-ANC Cyril Ramaphosa akitoa salamu za Black Power mwishoni mwa Kongamano la Kitaifa la 55 huko Johannesburg, Afrika Kusini, Jumanne, Desemba 20, 2022.AP

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC kimepuuza  ukosoaji wa uchimbaji madini inayohusishwa na tajiri mmoja wa Russia chini ya vikwazo vya Marekani.

Viktor Vekselberg ni mwekezaji katika United Manganese of Kalahari Ltd, ambayo mwaka jana ilichangia dola 826,000 kusaidia kufadhili mkutano wa uchaguzi wa ANC.

Wakosoaji wanasema mchango huo unadhoofisha madai ya chama ya msimamo usioelemea upande wowote kwa vita vya Ukraine na kukataa kwake kukosoa uvamizi wa Russia.

Mchango huo, wenye thamani ya randi milioni 15 kwa fedha za Afrika Kusini uliwekwa wazi hivi karibuni wakati tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini ilipotoa taarifa iliyoeleza kuhusu fedha zilizopokelewa na vyama vya siasa katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa 2022/23.

Alipoulizwa na VOA ikiwa mchango wa kampuni hiyo inayohusishwa na mshirika wa karibu wa Rais wa Russia Vladimir Putin uliathiri msimamo wa chama tawala kuhusu vita vya Ukraine, msemaji Mahlengi Bhengu-Motsiri alijibu kijuu juu.

ANC inapokea msaada wa fedha unaoombwa na ambao haujaombwa kutoka kwa vyama mbalimbali kote ulimwenguni, alisema kwa ujumbe mfupi wa simu. Baadhi hukubaliwa na wengine kurejeshewa ikibainika kuwa haiendani na maadili na sera za ANC. Msaada huu wa sasa utaangaliwa kwa mtazamo sawa na wengine.

Msimamo wa ANC juu ya mzozo wa Russia na Ukraine utabaki vile vile. Hatuamini kwamba kuna chochote kinaweza kupatikana cha maendeleo kutoka kwenye migogoro na vita. Bado tunazisihi pande zote kukutana na kutafuta suluhu bora zaidi.

Solly Malatsi msemaji wa kitaifa wa chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, aliukosoa mchango huo

"Hii inaelezea mtazamo wa serikali ya ANC kwa mzozo kati ya Russia na Ukraine ni kwa sababu inapata mamilioni ya randi kama michango kutoka kwa matajiri wa Russia. Inajitokeza mbele ya jitihada za Afrika Kusini za kutafuta na kuheshimu haki za binadamu kama mwanga unaoongoza sera yetu ya kigeni" aliongeza.

Fedha hizo zilienda kwenye kongamano la uchaguzi la ANC la Desemba ambapo Rais Cyril Ramaphosa alipewa muhula wa pili. Kumekuwa na matatizo katika ufadhili wa hafla hiyo, huku chama hicho chenye madeni makubwa kikipambana kukidhi gharama zake.

United Manganese of Kalahari, Ltd au UMK ni kampuni ya Afrika Kusini ambayo inachimba madini muhimu kwa uzalishaji wa madini ya chuma.

Mmoja wa wanahisa ni Kansela wa Baraza la Ufadhili la ANC, kulingana na ripoti za uchunguzi za vyombo vya habari vya Afrika Kusini, wakati kampuni ya Vekselberg inahusishwa na umiliki wa hisa nyingine ya chini ya asilimia 50 kwa ufanisi kuiruhusu UMK kuepuka vikwazo vya Marekani.

Mfanyabiashara huyo wa Russia ambaye anaripotiwa kuwa karibu na Ikulu ya Kremlin, alikuwa kwenye orodha ya vikwazo vya Marekani hata kabla ya uvamizi wa Ukraine mwaka jana. Baada ya vita kuanza, boti yake ya kifahari ilikamatwa na serikali ya Marekani na mali zake za Marekani zilipekuliwa na FBI.

Afrika Kusini, ambayo ina historia ya uhusiano wa karibu na Russia imejiepusha na kulaani uvamizi wa Moscow dhidi ya Ukraine kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Mchango huo unazua maswali kuhusu msimamo wa kisiasa wa Pretoria kuhusu vita vya Russia na Ukraine, alisema Steven Gruzd, mtaalam wa Russia katika Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini.

"Viktor Vekselberg amehusishwa na ANC hapo awali hii si mara ya kwanza kwa jina lake kujitokeza na huu ni mchango mkubwa kwa chama cha siasa chenye madeni makubwa.

Wanajaribu kuzungusha kwamba huu ni mchango wa kawaida, uendelezaji wa mchango mkubwa kwa chama cha siasa miongoni mwa vingine vingi, na kwamba watauchunguza ili kuona kwamba unaendana na maadili yao" aliongeza.

Mwezi uliopita, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa majeshi ya majini ya China na Russis kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika pwani yake ya mashariki, licha ya wasiwasi wa Marekani na Umoja wa Ulaya.

Mwezi Agosti, Putin anatarajiwa kuzuru Afrika Kusini kwa ajili ya mkutano wa kila mwaka wa BRICS - kundi la mataifa yanayoibukia kiuchumi yanayoundwa na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG