Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:38
VOA Direct Packages

China kuwajibishwa iwapo itahusika kwenye vita vya Ukraine, asema Chansela wa Ujerumani


Rais wa Marekani Joe Biden akifanya kikao na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Washington DRC. Machi 3,2023
Rais wa Marekani Joe Biden akifanya kikao na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Washington DRC. Machi 3,2023

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz Jumapili amesema kwamba hatua za uwajibikaji zitachukuliwa iwapo China itatuma silaha kwa Russia, ili kusaidia kwenye vita vya Ukraine, akiongeza kwamba anaamini kuwa China itajizuia kufanya hivyo.

Matamshi ya Scholz yamekuja kwenye mahojiano na televisheni ya CNN Jumapili, siku mbili baada ya kukutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini Washington DC. Mafisa wa Marekani katika siku za karibuni wameonya kuwa huenda China ikaanza kutoa misaada ya silaha kwa Moscow.

Kabla ya ziara yake ya Marekani, Scholz aliomba Beijing kujiepusha kutuma silaha kwa Russia na badala yake itumie ushawishi wake kurai taifa hilo kuondoa vikosi vyake nchini Ukraine. Baada ya kuulizwa na CNN iwapo China ingewekewa vikwazo kutokana na kutoa misaada kwa Russia, Scholz alijibu kwamba hilo lingekuwa na matokeo yake, bila kuweka bayana hatua ambayo ingechukuliwa.

Ujerumani ambayo ni uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya pia ndiyo mshirika mkuu zaidi wa kibiashara wa China.

XS
SM
MD
LG