Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 30, 2025 Local time: 10:34

Wahifadhi mazingira wakaribisha makubaliano ya mkataba wa kimataifa wa kulinda bahari


Jessie Cabagbag, 40, ambaye zamani alikuwa mwindaji haramu na sasa ni doria wa kasa wa baharini, akivuta wavu wake pamoja na mvuvi mwingine kwenye mashua yake huko Bacnotan, La Union, Ufilipino, Januari 11, 2023.REUTERS
Jessie Cabagbag, 40, ambaye zamani alikuwa mwindaji haramu na sasa ni doria wa kasa wa baharini, akivuta wavu wake pamoja na mvuvi mwingine kwenye mashua yake huko Bacnotan, La Union, Ufilipino, Januari 11, 2023.REUTERS

Wahifadhi wa mazingira walikaribisha makubaliano mwishoni mwa juma juu ya mkataba wa kimataifa uliopigiwa debe wa kulinda bahari na kukuza matumizi endelevu ya rasilimali kama vile mafuta yake, samaki na viumbe vingine vya baharini.

Washiriki katika mazungumzo hayo wanasema hii itawasaidia vyema wavuvi wanaohangaika barani Afrika na Kusini mwa Ulimwengu.

Machozi ya furaha yalionekana huko Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumamosi wakati wajumbe walikubaliana kuhusu mkataba wa kimataifa wa kuzuia unyonyaji wa rasilimali kwenye bahari kuu kuwa endelevu, baada ya kile mwanasayansi mmoja aliripotiwa kukiita mazungumzo muhimu zaidi ya kimataifa ambayo hakuna mtu aliyewahi kuyatarajia.

Kilichotokea katika Umoja wa Mataifa kinaweza kuwa na athari kubwa kote ulimwenguni, wataalam wanasema. Si haba kwa wavuvi barani Afrika kama Abdullah Hussein Mohammed, anayeishi pwani ya Sudan huko Bandari ya Sudan.

Abdullah pia husaidia kuendesha soko la ndani la samaki.

Anasema hifadhi ya samaki kote barani Afrika imekuwa ikipungua kwa miongo kadhaa sasa, jambo ambalo linaungwa mkono na takwimu za Umoja wa Mataifa. Yeye na jamii nzima wanateseka kutokana na hali hiyo.

Mkataba huo mpya unaangazia juu ya bahari kuu, sehemu yoyote ya bahari takriban maili 200 kutoka pwani, ambayo kwa kawaida haifikiwi na wavuvi wa Kiafrika.

Wataalamu wanasema kwamba uhifadhi wa mfumo wa ikolojia katika bahari kuu unamaanisha samaki zaidi na kwamba baadhi ya aina ya samaki ambao Mohammed anasema wametoweka pia sasa watapatikana karibu na nchi kavu, anakofanya kazi.

XS
SM
MD
LG