Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:08

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken awasili nchini Ethiopia

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili Addis Ababa Ethiopia Machi 14, 2023.REUTERS
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili Addis Ababa Ethiopia Machi 14, 2023.REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliwasili Jumanne jioni nchini Ethiopia kwa nia ya kuunga mkono mchakato wa amani baada ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili na kurejesha uhusiano na mshirika wake wa muda mrefu.

Safari ya Blinken katika taifa hilo la pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika inakuja ikiwa ni sehemu ya msukumo wa utawala wa Rais Joe Biden kuongeza uhusiano na bara la Afrika ambapo China na Russia zimekuwa zikiongeza ushawishi.

Ni ziara ya ngazi ya juu zaidi ya Marekani nchini humo tangu vita vilipozuka mwishoni mwa 2020 kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray na kuvuruga uhusiano wa Marekani na Addis Ababa huku Washington ikidai uhalifu dhidi ya binadamu.

Blinken anatarajiwa kukutana Jumatano mjini Addis Ababa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed mshindi wa nishani ya Amani ya Nobel ambaye wakati mmoja alionekana kuwa mstari wa mbele wa kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika wenye mtazamo wa mbele lakini ambao kwa haraka aligeuka karibu kuwa mtu wa kutengwa na Washington juu ya vita.

XS
SM
MD
LG