Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 02, 2023 Local time: 16:12

Kiongozi wa wengi katika Seneti ya Marekani Chuck Schumer amwonya Putin


Seneta Ron Wyden (D-OR) akimsikiliza Kiongozi wa Wengi katika Seneti Chuck Schumer (D-NY) akijadili bajeti ya Rais Biden katika mkutano wa wanahabari Capitol Hill huko Washington, Dc, Machi 9, 2023.REUTERS .

Kiongozi wa Wengi katika baraza la Seneti ya Marekani Chuck Schumer siku ya Jumanne aliita tukio lililosababisha kuanguka kwa ndege isiyo na rubani ya uchunguzi ya Marekani Reaper kitendo kingine cha ‘kutojali’ cha Rais wa Russia Vladimir Putin na jeshi lake.

“Nataka kumwambia Bw. Putin, Acha tabia hii kabla ya wewe kuwa sababu ya ongezeko la mzozo lisilotarajiwa Schumer “ alisema katika hotuba yake akifungua baraza la Seneti siku ya Jumanne.

Ndege isiyo na rubani ya uchunguzi ya jeshi la Marekani MQ-9 ilianguka huko Black Sea siku ya Jumanne baada ya kuvamiwa na ndege za kivita za Russia, likiwa ni tukio la kwanza kama hilo tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita.

Pentagon ilisema kuwa moja ya ndege za Russia aina ya Su-27 iliigonga propela ya ndege hiyo isiyo na rubani, na kuifanya isifanye kazi, huku wizara ya ulinzi ya Russia ikilaumu kukata kona kali kwa ndege hiyo isiyo na rubani kwa ajali hiyo na kusema kuwa ndege zake hazikugusana na ndege hiyo isiyo na rubani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG