Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 06:58

Wabunge wa Odinga wafunguliwa mashitaka Kenya


Waandamanaji wakiwazomea maafisa wa polisi wakati wa mkutano ulioitishwa na Raila Odinga tarehe 20, Machi 2023. Picha na YASUYOSHI CHIBA/AFP.

Wabunge wanne wa Kenya wameshtakiwa siku ya Alhamisi kwa kukutana kinyume cha sheria na kushiriki maandamano yaliyofanyika wiki hii dhidi ya serikali ya rais William Ruto kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, wakili wao Danstan Omari alisema.

Mtu mmoja aliuawa na wengine zaidi ya 200 walikamatwa wakati wa maandamano hayo yaliyo fanyika kitaifa yaliitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga siku ya Jumatatu.

Wabunge hao waliokamatwa ni pamoja na viongozi wa kundi la Odinga katika mabaraza yote mawili ya bunge, lakini waliachiliwa kwa dhamana, baada ya kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Nairobi, alisema wakili wao.

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi, Odinga alitaka kuachiliwa huru kwa wabunge hao, na kuionya kuhusu vitisho vinavyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano ya Kenya ya kufuta leseni za vituo sita vya televisheni vilivyo ripoti maadamano ambayo yalitakiwa kudhibitiwa.

Siku ya Jumatatu vituo hivyo vilirusha mubashara habari kwa saa kadhaa zikiwemo picha za polisi wakifyatua mabomu ya kutoa machozi na kuumwagia maji yanayowasha msafara wa Odinga.

Odinga mwenye umri wa miaka 78, ameitisha maandamano ambayo ameyataka yafanyike mara mbili kwa wiki, dhidi ya serikali, ikitaja kupanda kwa gharama za vyakula vya msingi kama vile unga wa mahindi ambao umesababisha mfumuko wa bei na bidhaa kuwa juu.

Pia kiongozi huyo wa upinzani anamshutumu Ruto kwa udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana, ukiwa ni mara yake ya tano mfululizo kwa Odinga kugombe nafasi ya urais nchini Kenya, katika uchaguzi huo alikuwa mshindi wa pili. Odinga alipinga matokeo hayo katika mahakama.

Chanzo cha habari hii ni shirka la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG